You are currently viewing KALIFAH AGANAGA MBIONI KUMALIZA BIFU YAKE NA MSANII BEBE COOL

KALIFAH AGANAGA MBIONI KUMALIZA BIFU YAKE NA MSANII BEBE COOL

Mwanamuziki wa dancehall kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga amemaliza tofauti zake na msanii Allan Hendrick ambaye ni kijana wa Bebe Cool kwa kufanya wimbo wa pamoja.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Aganaga amesema amechukua hatua ya kumaliza ugomvi uliokuwepo kati yake na familia msanii Bebe Cool kama njia kuwaomba msamaha watu wote aliowakosoa kwenye career yake ya muziki.

Hitmaker huyo wa “Kiboko” anaamini uhusiano wake na Allan Hendrick utamsaidia pakubwa kumfikia Bebe Cool ambaye kwa muda mrefu hajawakuwa na maelewano mzuri.

Utakumbuka Aganaga wamekuwa kwenye bifu na Bebe Cool baada kumsuta vikali kwa hatua ya kumtekeleza kimuziki mwanae Allan Hendrick ambapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa jambo lilomfanya mwanae huyo awe omba omba katika lebo ya muziki ya Gagamel kitendo kilichomkasirisha Bebe Cool.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke