You are currently viewing KAMATI YA GRAMMY WAFANYIA MABORESHO VIPENGELE VYA TUZO HIZO

KAMATI YA GRAMMY WAFANYIA MABORESHO VIPENGELE VYA TUZO HIZO

Kamati ya Tuzo za Grammy’s (Recording Academy) imefanya mabadiliko pamoja na maboresho kwenye Tuzo hizo ikiwemo kuongeza baadhi ya vipengele ambavyo awali havikuwepo.

Miongoni mwa machache ambayo Grammy’s wameongeza ni Tuzo ya Mwandishi bora wa nyimbo (Songwriter of The Year) ambapo sasa waandishi mahiri wa nyimbo watatunukiwa Tuzo kuanzia Tuzo za mwaka 2023. Kipengele kingine kilichoanzishwa ni (Song for Social Change) yaani wimbo ulioleta mabadiliko katika jamiii kupitia mashairi yake.

Lakini kubwa zaidi ambalo limeboreshwa ni (Album of the Year) ambapo sasa ili kuweza kuwa ‘eligible’ kupata nafasi ya kupenya kwenye kipengele hicho ni lazima nyimbo za Album hiyo ziwe zimechezwa (playing time) kwa 75% na nyimbo ziwe zimerekodiwa ndani ya kipindi cha miaka 5.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke