You are currently viewing KAMPUNI YA DIOR WASITISHA MKATABA WAO NA RAPA TRAVIS SCOTT

KAMPUNI YA DIOR WASITISHA MKATABA WAO NA RAPA TRAVIS SCOTT

Kampuni ya Fashion ya Dior imeamua kusitisha mkataba wake na Rapa Travis Scott, mkataba uliokuwa uanze mwakani 2022 kutokana na kisa kilichomkuta msanii huyo katika tamasha lake la Astro world ambapo watu 10 walipoteza maisha.

Kampuni hiyo imesema imefikia uamuzi huo kama heshima kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika Tamasha la Msanii huyo.

Hivyo, hakutakuwa na ushirikiano tena kati ya Kampuni hio kubwa ya usambazaji wa mavazi na msanii huyo. Huu ni muendelezo wa matukio ya kupoteza mikataba mbalimbali kwa Travis Scott baada ya Kampuni ya Anheuser-Busch kusitisha usambazaji wa vinywaji vya Cacti ambavyo ni vinywaji vya Travis.

Mbali na kupoteza mikataba, tayari mashtaka zaidi ya 100 yamefunguliwa dhidi ya msanii huyo kwa kufanya show isiyokuwa na tahadhari na hivyo kusababisha vifo vya watu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke