You are currently viewing KAMPUNI YA FACEBOOK KUBADILI JINA LA BRAND YAKE

KAMPUNI YA FACEBOOK KUBADILI JINA LA BRAND YAKE

Baada ya miaka 17 ya kuwepo kwa brand kubwa ya mitandao ya kijamii; Facebook inapanga kubadilisha brand na jina lake mwisho wa mwezi huu. Tetesi zilizovuja mtandaoni zinasema kwamba Mark Zuckerberg atatambulisha jina jipya la kampuni ya Facebook Oktoba 28 katika mkutano wa Annual Connect Conference 2021.

Malengo mapya ya Facebook ni kuingia katika teknolojia ya Metaverse na kuacha kuwa tu mtandao wa kijamii. Facebook ina malengo ya kukuza huduma za Instagram, WhatsApp na Uculus; kuhamia katika ulimwengu wa Virtual Reality na Augmented Reality.

Facebook haitakuwa kampuni pekee ya teknolojia ambayo imebadili brand yake. Mwaka 2015, Google ilibadilisha muunganiko wa kampuni zake na kuziweka chini ya Alphabet Inc na kuacha kuwa Search Engine tu.

Facebook itafanya branding mpya ya kampuni yake na kuweka malengo katika teknolojia ya metaverse ambapo watumiaji wake watawasiliana katika mitandao ya kijamii na katika virtual reality. Kampuni hiyo pia inalenga kuingia katika soko la saa, simu, VR, Metaverse na Games.

Hakuna anayefahamu jina la brand mpya ya Facebook, hata wakuu na viongozi wengi wa Facebook hawajaambiwa jina la kampuni kuu ambayo itasimamia social media platform na metaverse.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke