Kampuni ya Facebook hatimaye ameamua kubadili jina la mtandao wa kijamii wa Facebook na kuwa META.
Akizungumza kwenye mkutano wa kila mwaka wa kampuni hiyo, Annual Connect Conference Afisa Mtendaji Mkuu wa mtandao huo Mark Zuckerberg amesema kuwa hatua hii ni sehemu ya mabadiliko katika ruwaza yake kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kuelekea katika mfumo wa Metaverse ulimwengu wa kidigitali ambao unaweza kuwa na kizazi kijacho cha mitandao ya kijamii.
Mark amewaondoa watu shaka na kwa kusema kuwa mabadiliko hayo hayataathiri mitandao yake binafsi kama vile Facebook, Instagram na Whatsapp bali ni kampuni mama inayozimiliki.
Hata hivyo wapo ambao wameibuka kwa kumshutumu Mark kuwa anatupia jicho faida zaidi kuliko usalama