Licha ya kuwa mtumiaji maarufu, Snoop Dogg ni mwekezaji kwenye biashara ya bangi.
Kwa mujibu wa Bloomberg, kampuni ya Dutchie ambayo Snoop amewekeza pesa zake tangu mwaka 2018 imepanda thamani na kufikia takriban shillingi billioni 388.
Kampuni hiyo iliyopo Oregon nchini Marekani ilianza kufanya vizuri kifedha miezi saba iliyopita kwa kutajwa kuwa na thamani ya shillingi billioni 188 na imeendelea kukua siku hadi siku tangu kuhalalishwa kwa zao la bangi kwenye maeneo mengi nchini Marekani.
Ikumbukwe, mapema mwaka huu kampuni nyingine ya “Cannabinoid Technologies” ambayo Uncle Snoop amewekeza ilipanda thamani na kufikia shillingi billioni 7.5. Snoop pia ana bidhaa zake za bangi ziitwazo Leafs By Snoop.