Female rapper kutoka Kenya Kanambo Dede amerudi tena shuleni kuendeleza masomo yake ya upili baada ya kuacha shule miaka kadhaa iliyopita.
Rapa huyo ambaye alipata umaarufu nchini baada ya video yake kusambaa akiwa anachana mistari ya muziki wa hiphop aliacha shule kutokana na umaskini nyumbani kwao lakini pia mimba aliyoipata akiwa mchanga.
Akizungumza na mungai eve wakati wa uzinduzi wa tamthilia yake iitwayo Kamtupe nimsanye kanambo amesema ilikuwa ni matamanio yake kumaliza shule na kufanikisha ndoto zake maishani
” Since I moved out of Kayole, I felt I needed to go back to school and lay a foundation for my dreams since I feel I messed up in the past.”
Rapa huyo mchanga amewahimiza wanafunzi ambao tayari wapo mashuleni kutia bidii kwenye masomo huku akisema maisha mtaani ni magumu hivyo kwa wale ambao wana uwezo wa kupata elimu wachangamkie hiyo fursa.
Hata hivyo amesema atafanya kila awezalo kuhakikiaha anasoma lakini pia kwa upande mwingine anaendeleza kazi zake za muziki.
Ndoto za Kanambo dede kurudi shule imefanikishwa na uongozi wake wa Kaka Empire ambao umekuwa ukimuunga mkono kwenye shughuli zake za kimuziki ambapo mpaka ameshaachia ngoma tatu ambazo ni One Day, Wallahi, na Nataka Tena.