You are currently viewing KANYE WEST ADAI MUNGU ATAMRUDISHA MKEWE KIM KARDASHIAN

KANYE WEST ADAI MUNGU ATAMRUDISHA MKEWE KIM KARDASHIAN

Rapa kutoka Marekani Kanye West ‘Ye’ anaamini kwamba aliyewahi kuwa mke wake mwanamama Kim Kardashian, Mungu atatenda miujiza na kuwarudisha kuwa pamoja.

Kanye West amefunguka hayo alipokuwa akitoa misaada ya chakula kwa watu elfu 1 wenye uhitaji huko Jijini Los Angeles , ambapo amefunguka maneno ya busara pamoja na ya Imani ya kidini na kisha kuthibitiaha kwa mara ya kwanza yeye na Kim Kardashian hawapo pamoja.

Hii ni mara baada ya kusema kwamba kwa sasa yeye sio mume tena wa Kim ila anaamini ndoa yake na Kim kardashian ndio ndoa iliyokuwa yenye nguvu na ushawishi zaidi duniani, na hivyo wakirudiana basi itasaidia hata wengine walioko kwenye mahusiano.

Kanye West na Kim Kardashian ni wazazi wa watoto wanne ambao ni; North, Saint, Chicago, na Psalm, kwa sasa hawako pamoja huku sakata la talaka likienda mahakamani.

Hata hivyo tayari Kim Kardashian yupo kwenye mahusiano mapya na mchekeshaji Pete Davidson, uhusiano uliowekwa wazi hivi karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke