Rappa Kanye West ameingia tena kwenye headlines baada ya kushtakiwa mahakamani na kampuni ya Phantom Labs.
Kanye ameshtakiwa na Phantom Labs kampuni ya uandaaji matamasha kwa madai ya kutolipa $7.1m ambayo ni malipo ya matamasha matatu.
Inaelezwa licha ya kupokea barua nyingi za kukumbushwa kutoka kwa Phantom, Kanye West na timu yake wameendelea kwa njia isiyoeleweka kuinyima malipo kampuni hiyo.
Utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Kampuni ya “David Casavant Archive” ya kukodisha mavazi ilifungulia mashtaka mahakamani akidaiwa kukosa kurejesha mavazi aliyokodisha yenye thamani ya $400K.