Mamlaka ya mji wa California imemshtaki Rapa Kanye West kwa kile kilichoelezwa kwamba amevunja sheria za usafirishaji wa mizigo ambapo anadaiwa kuchelewesha bidhaa za YEEZY (shipping delays) ambazo watu huagiza mtandaoni.
Kanuni zinamtaka msafirishaji wa mizigo kutumia siku 30 tu kusafirisha mzigo na kumfikia mteja ndani ya siku hizo.
Mamlaka ya mji huo umesema Kanye West amekuwa akirudia mara kwa mara kukiuka sheria na kanuni hizo pasina kutoa maelezo yoyote ya maandishi kwa wateja, kurudisha pesa au hata kutoa ofa kama sheria inavyotaka.
Hadi sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa mtu mzima Kanye West na Kampuni yake juu ya madai hayo.