Mwanamama Kim Kardashian amefunguka kwamba baada ya kumalizika kwa Tuzo za Wall Street Journal’s Innovator Awards (WSJ), Kanye West alimuita pembeni na kumwambia kwamba amefanana na katuni “Marge Simpson” ambaye ni mhusika kwenye animation maarufu nchini Marekani, The Simpsons.
Kanye West hakuishia hapo, alienda mbali zaidi na kumwambia Kim kuwa amekwisha, jambo ambalo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda Kanye ametoa maneno hayo kutokana na namna ambavyo baby mama wake kim amekuwa akivalia kwenye matukio mbali mbali
Kauli ya Kim Kardashian imekuja siku chache baada ya kuweka wazi kuwa siku hizi amekuwa akipaniki hasa linapokuja suala la kupangilia mavazi tangu aachane na Kanye West.
Kama unakumbuka, Kanye West ndio alikuwa stylist wa Kim Kardashian na mara ya mwisho kumvalisha ilikuwa ni kwenye kipindi cha Saturday Night Live (SNL)