Rapa Kanye West ameamua kuwa mstaarabu kwa paparazzi ambao wamekuwa wakinasa matukio yake hasa akiwa kwenye mishe zake. Sasa Jana alionekana akimzuia Paparazzi mmoja ambaye alijaribu kumrekodi akiwa na mkewe Bianca Censori.
Kanye alimwambia Paparazzi huyo aache anachokifanya na kusema kwamba inabidi watu maarufu wawe wanapata asilimia fulani ya malipo kutoka kwenye picha na maudhui ambayo Paparazzi wamekuwa wakiyachukua kwao na kuuza au kuyatumia kwenye vyombo vyao vya habari.