Rapa Kanye West amelazimika kumpatia Kim Kardashian nyumba ambayo aliinunua mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yao ya Talaka ambayo yamefikia mwisho.
Rapa huyo kutoka Marekani atahamisha umiliki wa nyumba hiyo kutoka kwenye jina lake kwenda kwa Kim.
YE alinunua Jumba hilo Desemba 2021 kwa ($4.5 million) zaidi ya KSh. Milioni 551 likiwa pembeni ya makazi ya Kim Kardashian eneo la Hidden Hills ambapo alifanya hivyo kwa lengo la kuwa karibu na familia yake baada ya kuachana na mkewe.