Rapa kutoka Marekani Kanye West amerejea Instagram na kumtolea uvivu Pete Davidson ambaye hivi karibuni ametajwa kuachana na Kim Kardashian.
YE ameibuka na mfano wa taarifa kwenye gazeti la The New York Times ikidai Pete “Skete” Davidson kama ambavyo humtania, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 28.
Hii imekuja baada ya Mtangazaji huyo na Mchekeshaji kuripotiwa kubwagana na Kim Kardashian baada ya penzi lao kudumu kwa miezi 9.
YE aliingia kwenye mvutano wa mitandaoni na Pete baada ya kuingia penzini na Kim baada tu ya ndoa yao kuingia doa jeusi.