Rapa Kanye West anataka kila aliye karibu yake afanikiwe, amempa maua yake Drake akiwa hai.
Kwenye mahojiano mapya na Drink Champs, Kanye West amefunguka kwamba Drake ni rapa mkubwa na mkali zaidi kwa nyakati zote na hawezi kuomba radhi kwa kauli yake hiyo.
Hata hivyo YE amekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa watu mbali mbali duniani wakidai kuwa rapa huyo amekosa adabu kabisa kutomtaja Kendrick Lamar, Jay Z na Lil Wayne kama The Greatest Rapper Alive.
Licha ya kumwagia misifa Drake, Kanye ametema nyongo tena kwa Drizzy kwa kusema kuwa aliwahi kufanya mapenzi na Kris Jenner, Mama mzazi wa Kim Kardashian.