Staa wa muziki wa Hiphop kutoka nchini Marekani Kanye West ni kama amekubali yaishe kuhusu sakata la talaka na Kim Kardashian, ameona hawezi kumrudisha na sasa ameamua kumsogelea karibu ili apate nafasi ya kushirikiana naye kwenye malezi ya watoto wao.
Tovuti ya Daily Mail imeripoti kwamba Kanye West amenunua nyumba yenye thamani ya dolla millioni 4.5 ambayo ni takribani shillingi millioni 508 kwa pesa za Kenya iliyopo kando ya mtaa ambao anaishi Kim Kardashian na watoto wake.
Nyumba hiyo ipo kwenye eneo la mita za mraba 3,650 ikiwa na vyumba 5 vya kulala.
Kanye West na Kim Kardashian ni wazazi wa watoto wanne ambao ni; North, Saint, Chicago, na Psalm, kwasasa hawako pamoja huku sakata la talaka likienda mahakamani.
Hata hivyo tayari Kim Kardashian yupo kwenye mahusiano mapya na mchekeshaji Pete Davidson, uhusiano uliowekwa wazi hivi karibuni.