You are currently viewing Kanye West ashtakiwa kwa wizi wa wimbo

Kanye West ashtakiwa kwa wizi wa wimbo

Watu hawampumzishi Rapa KanyeWest kila siku wanampa msala mpya, Kampuni inayosimamia Kazi za B-Boy Records imedai kuwa Kanye West ameiba wimbo wa Boogie Down Productions wimbo unaitwa South Bronx ambao ulitoka Mwaka 1987.

Kanye West anadaiwa kuiba wimbo huo na kutumia kwenye Wimbo wake wa Life Of The Party aliomshirikisha Andre 3000 Unaopatikana kwenye Album yake ya DONDA kama Bonus Track.

Nyaraka zinasema kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote baina ya Kampuni hiyo na Kanye West kutumia Kazi hiyo.

Kupitia StepPlayer ya Kanye west ziliuzwa nakala 11000 ambapo inadaiwa YE aliingiza Mtonyo wa zaidi ya Dola Milioni 2 sawa na ziadi ya milioni 243 za Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke