You are currently viewing Kanye West atuhumiwa kuvunja simu ya shabiki

Kanye West atuhumiwa kuvunja simu ya shabiki

Rapa Kanye West ametajwa kama mtuhumiwa katika uchunguzi wa tukio la kihalifu. Hii inakuja mara baada ya kusambaa kwa video ikimuonesha Kanye akijibizana na paparazzi pamoja na shabiki. Video hiyo ilionesha kuwa kanye ni kama aliweuka ambapo alimjia juu shabiki huyo wa kike akidai kuwa amekuwa akimfuatilia na baada ya hapo alionekana akimpora simu shabiki huyo na kuitupilia mbali.

Lakini pia kanye anaoneshwa kukerwa sana sehemu mbalimbali na tabia za paparazzi ambao wamekuwa wakimfuatilia mpaka kwenye maisha yake binafsi. Sasa kwenye video hiyo pia Kanye anaonekana akiwaambia paparazzi kwamba anataka kuwaona watoto wake bila ya wao kumpiga picha. Kanye alikuwa anaenda kuwaona watoto wake kwenye mchezo wa basketball.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke