You are currently viewing KANYE WEST AWAFUTA KAZI MAFUNDI WA MITAMBO WALIOANDAA ONESHO LAKE LA DONDA 2 EXPERIENCE CONCERT

KANYE WEST AWAFUTA KAZI MAFUNDI WA MITAMBO WALIOANDAA ONESHO LAKE LA DONDA 2 EXPERIENCE CONCERT

Microphone ilimzingua sana rapa Kanye West wakati akitumbuiza Jukwaani,ambapo aliamua kuitupa kwa hasira kwenye maji. Rapa huyo alikuwa akitumbuiza kwenye Onesho la ‘Donda 2 Experience Concert’ lililofanyika februari 23 mjini Miami.

Tatizo la microphone kusumbua liliripotiwa na baadhi ya kurasa za mitandao ya Kijamii na wadau waliokuwa wanafuatilia onesho hilo mtandaoni.

Hata hivyo Kanye West ameripotiwa kuwafuta kazi kamati yake ya ufundi iliyokuwa ikishughulikia performance yake kwenye ‘Donda 2 Experience Concert’.

Ikumbukwe Kanye west alipata nafasi ya kuwasikilizisha mashabiki zake midundo ambayo itapatikana kwenye DONDA 2 album ambapo baadhi ya wasanii walioshirikishwa ni pamoja na; XXXTENTACION, Don Toliver, Baby Keem, Quavo, Offset, Future, Travis Scott, Playboi Carti, Jack Harlow, Sean Leon, Soulja Boy, Fivio Foreign na Alicia Keys.

Donda 2 Album tayari imeshatoka ikiwa na jumla ya mikwaju 14 na inapatikana kwenye  jukwaa lake la ‘Strem Player’,  kifaa maalum cha kusikiliza muziki

Huu ni muendelezo wa album yake Donda ambayo ilitoka Agosti 29 mwaka 2021.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke