Rapa Kanye West amejipata njia panda kwenye mitandao ya kijamii baada ya sakata la kuweka na kuuza kwenye mfuko wa takataka mavazi yake mapya toleo la Yeezy GAP.
Aina hiyo ngeni ya uuzaji ambayo wengi wameitafsiri tofauti na walivyozea kuona mavazi yakiwa yametundikwa kwenye hanger, imepelekea wengi kumtaka YE aombe radhi kwani ni kama dhihaka.
Sasa FOX NEWS wamempata YE na kuzungumzia suala hilo ambapo amesema “Mimi ni mngunduzi, sipo hapa kukaa na kuomba radhi juu ya mawazo (ideas) yangu.” amesema YE ambaye anadaiwa kuwa alimletea noma mtu wa mauzo wa Kampuni ya GAP mara baada ya kuona ametumia hanger kuonesha nguo hizo.