You are currently viewing KANYE WEST AWEKEWA VIKWAZO KUINGIA KWENYE BIRTHDAY  PARTY YA BINTI YAKE, CHICAGO WEST

KANYE WEST AWEKEWA VIKWAZO KUINGIA KWENYE BIRTHDAY PARTY YA BINTI YAKE, CHICAGO WEST

Kanye West ameamua kuanika wazi kila kitu ambacho kinaendelea baina yake na Kim Kardashian, usiku wa kuamkia leo ameeleza namna ambavyo aliwekewa vikwazo kuingia kwenye birthday party ya binti yake, Chicago West.

YE anadai kwamba hakupewa kabisa location ya wapi party hiyo itafanyika,ila juhudi za Travis Scott zilisaidia kwani alimtumia location na alifika eneo hilo ambapo kulikuwa na party pia ya Stormi Webster.

Stori kubwa ni kwamba baada ya kufika, walinzi wa Kim Kardashian walimzuia YE kuingia ndani ya party hiyo kitendo ambacho kilimkasirisha sana. Shukrani kwa Kylie Jenner kwani alimpambania hadi akafanikiwa kuingia na kufurahi pamoja na binti yake.

Kwenye video ambayo anaonekana akizungumzia sakata hilo, YE anasema Kim anatengeneza mazingira watoto wake wamuone kama baba asiyejali.

Hata hivyo sakata la Kanye kuzuiwa kuwa karibu na watoto wake halijaanza jana, kwenye mahojiano na Hollywood Unlocked, Kanye West alisema Jumatatu iliyopita aliwafata watoto wake shule ili kuwapeleka nyumbani, alipofika shuleni walinzi wa Kim Kardashian walimzuia getini.

Hakubishana nao, siku nyingine alifanikiwa na kuwafikisha hadi nyumbani na North alimtaka aingie ndani lakini walinzi walimzuia, inadaiwa kuwa Pete Davidson ambaye ni mpenzi mpya wa Kim, alikuwepo ndani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke