Rapa kutoka Marekani Kanye West amekuwa mfano na sehemu ya Wanafunzi kujifunza.
Rapa huyo ameingia kwenye mtaala wa elimu kwa kuwekwa kwenye Kitabu cha somo la Historia kwa Wanafunzi wa Sekondari nchini Marekani.
Kikao chake na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump katika Ofisi ya Rais (Oval Office) ndani ya Ikulu ya White House mnamo Oktoba 11, mwaka 2018 kimeingizwa kwenye mtaala wa Somo la Historia kwenye Topic isemayo: US Democracy and Participation.