You are currently viewing SHEEBAH AFUNGUKA CHANZO CHA UCHAGUZI WA UMA KUAHIRISHWA

SHEEBAH AFUNGUKA CHANZO CHA UCHAGUZI WA UMA KUAHIRISHWA

Mwanamuziki Sheebah Karungi amefunguka sababu zilizopelekea uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA kuahirishwa.

Kwenye mahojiano na Bukedde TV Sheebah amesema yeye ndiye aliwashawishi wasanii kususia upigaji kura kwa njia ya SMS kwenye uchaguzi huo ambao ulikumbwa na dosari.

“Mimi nilichangia uchaguzi huo kufutwa, nilikuwa kwenye simu nikiwashawishi wadau mbalimbali kususia uchaguzi, nashukuru kamati ya uchaguzi ilisikiliza malilio yetu, sielewi ilikuwaje wafuasi wa King Saha washindwe kupiga kura kutokana na mtandao huo kuharibika na bado kura zote za Cindy zilikuwa zinaendelea kutiririka. Huo ulikuwa udanganyifu uliopitiliza,” alisema.

Inadaiwa Sheebah ndiye anamfadhili kifedha King Saha kusambaratisha juhudi za Cindy Sanyu kutua uongozi wa chama cha wanamuziki nchini uganda kwa mara ya pili.

Sheebah anajiunga na orodha ya wanamuziki kama Ykee Benda, Fefe Bussi, King Micheal, Spice Diana, Karole Kasita, Jose Chameleone, na Eddy Kenzo wanaoendelea kumshutumu Cindy Sanyu kwa kutumia vibaya pesa za wasanii kwa manufaa yake binafsi.

Utakumbuka Uchaguzi wa UMA uliahirisha Juni 6 mara baada ya wafuasi wa King Saha kudai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi hadi sasa Kamati ya inayojishughulisha na uchaguzi hajatoa mweelekeo kama uchaguzi utarudiwa ila jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke