Rapa Kanye West ameripotiwa kuwa penzini na mrembo Candice Swanepoel kutoka Afrika Kusini.
Wawili hao walionekana pamoja kwenye maonesho ya New York Fashion Week wakiwa kwenye huba zito.
Kwa mujibu wa TMZ, YE na Candice walionekana wakicheka na kufurahi pamoja na mchekeshaji Chris Rock huku wakipiga picha na baadaye walipanda gari moja na kuelekea hotelini.
Hata hivyo mtandao wa Page Six umeripoti kwamba inaweza kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi bali ni kiki tu za ku-promote miwani za Yeezy ambazo mrembo huyo ni sura ya bidhaa hizo.