Rapper kutoka nchini Marekani Kanye West ametajwa kuwa kwenye mahusiano mapya na mwanamitindo Channey Jones.
Tovuti mbalimbali Marekani zinasema kuwa, Kanye West amekuwa katika mahusiano ya siri na mrembo huyo kwa muda sasa.
Uvumi wa Mahusiano yao ulianza kuvuma baada ya Kanye West kuonekana na Mwanadada huyo huko Calfornia, nchini Marekani Februari 9 Mwaka huu.
Kumbuka ni wiki mbili tu nyuma zimepita tangu mtu mzima Kanye West abwagane na aliyekuwa mpenzi wake Julia Fox.