Rapper Kanye West amedokeza mpango wa kuja na filamu ya maisha yake.
Kanye amemuomba mwigizaji Danny McBride kuvaa uhusika wake na kucheza filamu hiyo.
McBride amethibitisha taarifa hiyo kwenye podcast ya Jimmy Kimmel Live kwenye mtandao wa Youtube kwa kusema kwamba YE alimpigia simu na kumpa ombi hilo.
Mwigizaji huyo ambaye pia ni mchekeshaji wa nchini Marekani amesema alilipokea kwa mikono miwili wazo hilo la Kanye West.
Utakumbuka Danny McBride alipatia umaarufu mkubwa kwenye Dunia ya filamu kwa kazi zake kali ikiwemo; Eastbound & Down, Good Vibes, The Righteous Gemstones, The Heartbreak Kid, Tropic Thunder, 30 Minutes or Less na nyingine kibao.