Rapa Kanye West amesema kuwa ana mpango wa kununua Kampuni kubwa ya viatu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram YE ameuliza kuwa kama kuna kampuni yoyote kubwa ya viatu itapendezwa na ombi lake ifanye mawasiliano nae.
Kanye West amesisitiza kuwa anahitaji kununua Chapa kubwa kama alivyofanya James Salter kununua kampuni ya REEBOK.
Mbali na hilo rapa huyo amesema kuwa alijaribu kuzungumza na Kampuni ya JB MORGAN lakini haijawezekana kupata dili kwani wana mkataba na kampuni ya ADIDAS.