Rapa Kanye West na Big Sean wamemaliza tofauti zao, wameonekana wakiingia studio pamoja.
Kwenye picha zinazotembea kwenye mitadao ya kijamii wameonekana pia French Montana, Pusha T, Pressa, Fivio Foreign and The Game.
Tetesi zinadai kwamba Kanye west yupo kwenye maandalizi ya album yake ijayo ‘Donda 2’ na huwenda sauti za wakali hao zikasikika kwenye album hiyo.
Big Sean na Kanye west waliingia kwenye vita ya maneno mwishoni mwa mwaka jana, hii ni baada ya Kanye west kusema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ni kumsaini Big Sean.
Baada ya kuruka interview hiyo ambayo Kanye west alifanya kwenye Podcast ya ‘Drink Champs’ Big Sean aliomba kukaa kwenye kiti hicho pia na kumjibu Kanye west kwa kusema yote aliyozungumza ni upuuzi mtupu japo heshima yake kwake haiwezi kupotea.
Big Sean ambaye aliondoka GOOD Music na kuanzisha label yake, anamdai Kanye zaidi ya shilling million 147 za Kenya.