You are currently viewing KANYE WEST NA BILLIE EILISH WATAJWA  KUWA VINARA KWENYE TAMASHA LA COACHELLA 2022

KANYE WEST NA BILLIE EILISH WATAJWA KUWA VINARA KWENYE TAMASHA LA COACHELLA 2022

Rapa Kanye West pamoja na msanii mwenzake Billie Ellish wametajwa kuwa watakuwa wasanii vinara kwenye tamasha la maarufu la muziki nchini Marekani, Coachella mwaka wa 2022. Chanzo kimoja kimeuthibitishia mtandao wa Variety kuhusu taarifa hii.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Kanye West kuwa msanii kinara kwenye tamasha hilo kubwa, mwaka 2011alifanya hivyo tena huku Billie Ellish pia akihusika mwaka 2019 akiwa binti mdogo tu.

Tayari tiketi zote zimemalizika huku ikitajwa tiketi 125,000 zimeuzwa kwenye onesho la siku ya kwanza.

Ikumbukwe kwamba Coachella ya mwaka huu imepangwa kufanyika wikendi ya April 15-17 na kumalizika wikendi ya April 22-24 mwaka wa 2022.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke