Baada ya kumaliza bifu lao la miaka kadhaa wakali Kanye West ‘Ye’ na Drake wanatarajia kufanya tamasha la pamoja huko Los Angeles nchini Marekani katika viwanja vya Memorial Coliseum’s.
Wawili hao watapanda kwenye jukwaa la tamasha hilo linalotambulika kama “Free Larry Benefit Concert” Desemba 9, mwaka wa 2021.
Tamasha hilo ni mahususi kwa ajili ya kupaza sauti za kumuacha huru Larry Hoover ambaye yupo gerezani huko mjini Florence, Colorado nchini Marekani akitumikia kifungo cha miaka 150 hadi 200, ambacho alikianza mwaka 1973 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.