You are currently viewing KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WARUSHIANA MANENO MAKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM

KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WARUSHIANA MANENO MAKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM

Rapa kutoka Marekani Kanye West ameonesha kutokupendezwa na kitendo cha Mwanae wa kike North West aliyezaa na mrembo Kim Kardashian kujiunga katika mtandao wa TikTok.

Kupitia instagram page yake Kanye West ameibuka na kuomba ushauri ni kitu gani afanye juu ya hili la mwanae kuungwa kwenye mtandao huo maarufu wa TikTok

“Hii Ni Talaka Yangu Ya Kwanza, Nahitaji Kufahamu Ni Kipi Nifanye Kuhusu Mwanangu Kuunganishwa Katika Mtandao Wa Tiktok Kinyume Na Mapendekezo Yangu”

Baada ya Kanye West kuhoji na kuomba ushauri nini afanye baada ya mwanae kuwepo kwenye mtandao maarufu wa TIKTOK sasa mama wa North ambaye ni Kim Kardashian ameamua kumjibu Kanye West juu ya hilo.

Kupitia Insta story ya Kim Kardashian amemjibu kudai kuwa Kanye West anawaumiza watoto kwa kuleta tofauti zao kwenye mitandao ya kijamii.

“Mashambulizi ya Kanye West juu yangu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni mabaya na yanaumiza zaidi kuliko mtoto kutumia mtandao wa TikTok.

“Kama Mzazi na Muangalizi wa Mtoto wetu , nahakikisha nampa malezi bora huku nikimpa uhuru wa kuonyesha Vipaji Vyake Mbalimbali alivyonavyo . Talaka ni kitu kibaya kwa watoto wetu , Lakini vitendo vya Kanye West Kutoka kutuendesha vinaongeza maumivu zaidi kwenye Maisha yetu ”

Hata hivyo bado Rapa Kanye West amelishikilia swala la Mwanae North kuwepo kwenye mtandao wa TikTok ambapo ameweka Taratibu na Sheria za kujiunga na mtandao huo.

YE ameweka maelezo ya kujiunga na mtandao huo ambapo moja ya sheria ni mtoto mwenye umri wa miaka 13 na kushuka chini inabidi ajisajili kwa umri wake ili apate kuona maudhui yanayomfaa tu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke