Ndoa ya Kim Kardashian na Kanye West imevunjika rasmi baada ya miaka 8.
Mchakato wa talaka umekamilika Machi 3 na Jaji wa mahakama ya mjini Los Angeles ametangaza rasmi kwamba Kim Kardashian anaweza kuendelea na maisha yake ya U-single lakini pia ameondoa jina la ‘West’ kwenye majina yake matatu.
Tovuti ya TMZ imebaini kwamba hakuna tumaini lolote kwa Kim na Kanye West kurudiana kwani Kim amepigilia msumari kwenye maandishi kwamba jambo hilo haliwezekani kwa sasa.
Kim Kardashian amesema alifanya kila awezalo kuyamaliza na Kanye West tangu afungue shauri la talaka mwezi Februari mwaka 2021 lakini Ye hakuonesha ushirikiano.
Ikumbukwe Kim na rapa Kanye West wamedumu kwenye ndoa kwa takriban miaka 7 na amejaliwa watoto wanne ambao ni Psalm, Saint, Chicago na North.