You are currently viewing KANYE WEST NA UNIVERSAL MUSIC GROUP WABURUZWA MAHAKAMANI

KANYE WEST NA UNIVERSAL MUSIC GROUP WABURUZWA MAHAKAMANI

Rapa kutoka Marekani Kanye West pamoja na Universal Music Group wanakabiliwa na kesi ya wimbo wa “Power” alioutoa mwaka 2010.

Kwenye wimbo huo, Kanye West alitumia vionjo kutoka kwenye wimbo wa King Crimson “21st Century Schizoid Man,” wa mwaka 1969,.

Kwa mujibu wa Variety, Declan Colgan Music Ltd, ambao wanamiliki toleo la awali la wimbo huo, waliwasilisha kesi katika mahakama kuu ya Uingereza mapema mwezi Machi 2022.

Madai hayo yanakuja kufuatia Kanye West kuweka wimbo huo kwenye mtandao wa Youtube mwaka 2010 kabla ya kuwepo kwa makubaliano ya awali ya matumizi ya sampuli hiyo ambapo wimbo huo mpaka sasa umepata jumla ya watazamaji takriban milioni 134.

Inaelezwa wakati huo Declan Colgan Music Ltd ilimuomba Ye, na kampuni yake ya uzalishaji, Rock the World kutia saini mkataba ambao ulisema sampuli hiyo itapata mrabaha wa 5.33% katika kila sehemu ambayo nakala ya wimbo wa huo itauzwa au kutumiwa kwa namna yeyote.

Declan Colgan Music Ltd, sasa inadai kwamba Universal Music Group imeshindwa, na inaendelea kushindwa, kutii wajibu wake wa kihasibu wa mrabaha kuhusiana na masharti sahihi waliyopaswa kuyafuata.

Kwa mujibu wa Complex, kwa Sasa wanachotaka Declan Colgan Music Ltd ni mirabaha yao ya Streaming Royalties iwe sawa na mauzo halisi ya CD, badala ya asilimia zinazotolea na majukwaa ya malipo kama Spotify kwa kila stream moja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke