You are currently viewing KAPA CAT AKIRI HADHARANI KUCHUKIA MIPIRA YA KONDOMU

KAPA CAT AKIRI HADHARANI KUCHUKIA MIPIRA YA KONDOMU

Msanii asiyeishiwa na vituko kila leo Kapa Cat amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kukiri hadharani kuwa anachukia kutumia kondomu wakati wa tendo la ndoa.

Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni mrembo huyo ambaye anadaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda amesema anafadhalisha kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga kwa kuwa mipira ya kondomu humwasha sana kwenye sehemu zake za siri.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “You Guy” ameenda mbali na kudai kuwa kipindi cha nyuma alikuwa na mazoea ya kupima HIV kila baada ya miezi mitatu lakini daktari alipogundua yuko njia panda kiafya alimshauri kujenga tabia ya kujua hali yake kila baada ya miezi miwili.

Kapa Cat alipata umaarufu kwenye muziki wake mwaka wa 2018 kupitia wimbo wake uitwao “Sikyo” na tangu wakati huo amekuwa akisuasua kwenye suala la kuachia hitsongs.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke