Mwanamuziki kutoka Uganda Kapa Cat ameitaka wizara ya elimu kutoingilia namna wasanii wanavyovalia mavazi yao.
Akizungumza kwenye moja ya show yake Kapa Cat amesema hatua ya wizara hiyo kuwafungia wasanii kufanya show zao mashuleni, inawanyima uhuru wa kuwa wabunifu kwenye suala la kuendeleza sanaa yao.
Utakumbuka mwezi mmoja uliopita wizara ya elimu nchini iliwapiga marufuku kutotumbuiza mashuleni kutokana na baadhi ya wasanii wa kike kuvalia mavazi yanayokwenda kinyume na maadili ya jamii.
Hata hivyo mpaka sasa wasanii hawajui ni lini hasa serikali itawaruhusu kutumbuiza mashuleni.