You are currently viewing Karen Nyamu afunguka baada ya kuzua tafrani nchini Dubai

Karen Nyamu afunguka baada ya kuzua tafrani nchini Dubai

Baby Mama wa mwanamuziki wa Mugithi Samidoh Muchoki, Karen Nyamu amezungumzia kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akiwa anasindikizwa na walinzi nje ya ukumbi wa tamasha la Samidoh huko Qatar.

Akizungumza moja kwa moja kwenye mtandao wa Instagram, Karen Nyamu amesema hakuwa na habari kuwa alihitaji leseni ya kuonekana jukwaani.

Katika utetezi wake, amesema hakufanya kosa lolote kwenda jukwaani kwani alikuwa akifurahia tu burudani kama mashabiki wengine.

Seneta huyo mteule ameongeza kuwa chini ya shinikizo ya kilevi, hivyo maazimio yake ya 2023 ni kuacha kunywa pombe kabisa.

“Pombe inanifanya nisahau njia, Nimeacha Pombe.”

Kwenye instagram live, shabiki mmoja alimshauri aache kufuata Samidoh ambapo alijibu kwamba anahitaji maombi ili kukomesha mzaha maishani mwake.

Karen Nyamu pia aliwataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi naye.

“Niko na Kila kitu kitu sina ni haya.”

Akijibu moja ya shabiki yake, aliongeza kuwa hana mpango wa kuachana na Samidoh kwa sababu ya malezi ya watoto wao wawili kwa pamoja.

“Simuachi, lazima Tulee watoto.”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke