You are currently viewing Karen Nyamu azua purukushani kwenye tamasha la Samidoh Dubai

Karen Nyamu azua purukushani kwenye tamasha la Samidoh Dubai

Seneta mteule  Karen Nyamu amejipata katika hali ya aibu baada ya kujaribu kujiunga na baba wa mtoto wake Samidoh Muchoki jukwaani alipokuwa akitumbuiza nchini Dubai.

Kwenye video inayosambaa sana katika mitandao ya kijamii, Karen Nyamu ameonekana akivamia jukwaa ambalo Samidoh alikuwa akitoa burudani kwa mashabiki katika jaribio la kujiunga na mwanamuziki huyo wa Mugithi.

Samidoh hata hivyo hakumpa muda wa kuzua purukushani ambapo walinzi wake walimsindikiza Karen Nyamu nje.

Katika video hiyo, Samidoh alisimama akiwatazama maafisa wa usalama wakimsindikiza mama ya mtoto wake nje. Kisha akamkumbatia mkewe Edday Nderitu kwa upendo huku wakipiga picha na mashabiki.

Siku chache zilizopita, Samidoh na mkewe walisafiri nchini Dubai kwa ajili ya hafla ya sherehe ambapo alitarajiwa kutumbuiza pamoja na wanamuziki wengine. Mama ya mtoto wake Karen Nyamu pia alijikatia tiketi ya ndege kujiunga nao kwenye sherehe hiyo ya mwisho wa juma.

Mashabiki wengi walikasirishwa na hatua ya Karen kuhujumu safari ya Samidoh-Edday kwa kusema kwamba alimkosea heshima mke mkuu wa mwanamuziki huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke