Nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema, ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kimataifa, akiwatakia kila la kheri Ufaransa huku akiomba radhi pale alipokosea na kujipongeza pale alipofanya vyema.
Benzema amefunguka hayo ikiwa leo ni siku yake ya kumbukizi ya kuzaliwa ambapo ametimiza umri wa miaka 35. Amehitimisha safari yake ndani ya timu hiyo akiwa amecheza jumla ya mechi 97 na kufanikiwa kupachika mabao 37.