You are currently viewing KAROLE KASITA APINGA HATUA YA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU WASANII KUTUMBUIZA MASHULENI

KAROLE KASITA APINGA HATUA YA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU WASANII KUTUMBUIZA MASHULENI

Msanii Karole Kasita amekosoa hatua ya wizara ya elimu nchini Uganda kuwapiga maarufuku wasanii kutumbuiza kwenye shule za umma kutokana na wao kuvalia mavazi yao yanayokwenda kinyume na maadili ya jamii.

Karole Kasita amesema wizara ya elimu nchini Uganda inapaswa ije na njia nyingine kushughulikia swala la wasaniii kuvalia vizuri wakiwa jukwaani kwani inahujumu kazi za wasanii ikizingatiwa wengi wao wanategemea muziki kupata riziki.

Wasanii wengine ambao wameonekana kutoridhishwa na kitendo cha Wizara ya Elimu kusitisha maonesho mashuleni kutokana na wasanii kutovali mavazi yenye staha ni pamoja na Pia Ponds na Rickman Manrick.

Utakumbuka mapema wiki hii wizara ya elimu nchini Uganda ilisitisha maonesho ya muziki mashuleni hadi pale watakapotoa mweelekeo wa namna  wasanii wanapaswa kuvalia wakiwa kwenye majukwaa ya shule.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke