Mwanamuziki kutoka Uganda Karole Kasita amedai kwamba hatoshiriki uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini humo ambao utafanyika mwezi huu.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Karole Kasita amepuzilia mbali uchaguzi huo kwa kusema kwamba wagombea wa nyadhfa za uongozi katika chama hicho hawana ajenda za kuwasaidia wasainii wa uganda kwani wengi wao wanalenga kujinufaisha wenyewe.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Balance” amesema hatashiriki uchaguzi wa chama cha wasanii nchini uganda hadi pale chama hicho kitaanza kuangazia maslahi ya wasanii.
“Sitapiga kura wala kushiriki katika masuala ya chama hadi watakapokuwa tayari kusaidia tasnia hiyo. Wengi wao wanatafuta pesa kutoka kwa serikali, hawaujali sisi,” alisema.
Utakumbuka Cindy Sanyu na King Saha wanawania nafasi ya urais katika Chama cha Wanamuziki nchini Uganda (UMA).