You are currently viewing KAROLE KASITA WAZOZANA NA MENEJA WAKE JORAM KISA PESA

KAROLE KASITA WAZOZANA NA MENEJA WAKE JORAM KISA PESA

Karole Kasita alianza kuimba akiwa shule ya upili ya St. Joseph Naggalama ambapo alirekodi wimbo wake wa kwanza uitwao  “Bounce it” kwa ushirikiano na msanii Nutty Neithan mwaka wa  2015 akiwa chuo kikuu.

Lakini baada alijuunga na bendi ya muziki ya S &  S kabla ya kuanza muziki wake kama msanii wa kujitegemea mwaka wa 2018.

Karole ambaye anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kutoa burudani ya nguvu akiwa jukwaani ameweka alama kwenye tasnia ya muziki nchini uganda kama moja kati ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri.

Ufanisi huo umetokana na mchango wa Meneja Joram ambaye amekuwa akisimamia muziki wake kwa muda lakini taarifa mpya ni kuwa mrembo hafanyi kazi tena na meneja wake huyo.

Chanzo cha karibu na karole kasita kinasema msanii huyo na meneja wake waliingia kwenye ugomvi kutoka na mzozo wa fedha jambo lilomlazimu mrembo huyo kujiondoa na kuanza kufanya muziki wake kivyake.

“They are no longer working together. They fell out and it could be due to money,” the source revealed.

Hata hivyo mpaka sasa Karole Kasita pamoja na aliyekuwa meneja wake wapo kimya juu ya suala hilo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke