You are currently viewing KATE ACTRESS ALAMBA SHAVU YA UBALOZI NICE & LOVELY KENYA

KATE ACTRESS ALAMBA SHAVU YA UBALOZI NICE & LOVELY KENYA

Mwigizaji maarufu nchini Kate Actress amelamba dili nono la ubalozi wa vipodozi vya Nice & Lovely kwa upande wa Kenya.

Kate Actress ametangaza habari njema kwa wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kubwa kujiunga na familia ya Nice & Lovely ambayo inazalisha bidhaa za Urembo za asili zenye uwezo wa kupendezesha ngozi bila ya madhara.

Kate Actress amesema vipodozi hivyo vya asili havina kemikali inayoharibu ngozi na kwamba vimethibitishwa na mamlaka husika kutumika kwa wanaume na wanawake.

“Nasiwezi jizuia ….. 😭🙏 We did it my watuz , you all kept manifesting this for me ,it’s here 🙏. The official face of @niceandlovelykenya .
#lorealkenya” 

Kwa upande wake Kampuni Nice & Lovely kupitia mitandao yao ya kijamii imemkaribisha mwigizaji huyo kufanya nao kazi huku ikisema kuwa ina furaha ya kuingia ubia nae kwa kuwa atawaongezea wateja kutokana na watu wengi wanaomfutilia kwenye mtandaoni.

“Today was one for the books! We unveiled the one, the only @kate_actress as our official brand ambassador🎊🎉. We are so proud and honoured to have her as part of the family and we can’t wait to go on this journey together. #NiceandLovelyUnveiling”

Hata hivyo inaonekana Milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwa Kate Actress kwani ukiachilia mbali kuwa balozi wa bidhaa hizi za urembo za kimataifa pia ni balozi wa Harpic Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke