Mwanamuziki Kaz Lucas amewajibu wanaotaka kuanika picha zake za utupu baada ya kukiingia kifua klabu moja ya usiku iitwayo Alchemist iliyoko jiji Nairobi kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram amesema ameshangazwa na namna watu wameanza kumdhalalisha kutokana na maoni yake juu night club hiyo huku akisema yeyote anayetaka kuchapisha picha zake za utupu ana ruhusa ya kufanya hivyo kwa kuwa hajutii matamashi aliyotoa kuhusu Alchemist.
Kauli ya Kaz imekuja mara baada ya watu kumshambulia alipoanza kuwalaumu watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kuchochea serikali kufungwa Alchemist ambayo ilikuwa imetoa ajira kwa wakenya wengi.
Wiki iliyopita video ilisambaa mtandaoni ikimuonyesha jamaa moja mwenye asili ya kiafrika akitimulia kwenye eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya wazungu jambo ambalo lilipelekea wakenya kukashifu vikali kitendo hicho cha kibaguzi.