You are currently viewing KAZ LUCAS AWAPA SOMO WATUMIAJI WA MITANDAO KWA KUCHANGIA KUFUNGWA KWA ALCHEMIST

KAZ LUCAS AWAPA SOMO WATUMIAJI WA MITANDAO KWA KUCHANGIA KUFUNGWA KWA ALCHEMIST

Mwanamuziki Kaz Lucas amesikitishwa na hatua ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kupelekea eneo la burudani la Alchemist liloko jijini Nairobi kufungwa kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Kaz amedai kufungwa kwa eneo hilo kumepelekea maelfu ya wakenya kukosa kazi jambo ambalo amesema limetokana na baadhi ya watu kwenye mitandao ambao hawana huruma kwa shughuli za watu.

Aidha amewataka wakenya kutumia mitandao ya kijamii kwa busara badala ya kuwaharibia watu riziki yao kutokana na wao kuamini uvumi unaoenezwa na wambea.

Kauli ya Kaz Lucas imekuja mara baada ya Alchemist kufungwa kwa madai ya kuwabagua wateja wao kwa misingi ya rangi.

Mapema wiki hii video ilisambaa mtandaoni ikimuonyesha jamaa moja mwenye asili ya kiafrika akitimulia kwenye eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya wazungu jambo ambalo lilipelekea wakenya kukashifu vikali kitendo hicho cha kibaguzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke