Msanii kutoka nchini Kenya Kelechi Africana anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumtelekeza mtoto wake.
Akizungumza na Msenangu FM baby mama wa msanii huyo anayejulikana kama Shinaz Shaz amedai kwamba msanii huyo amekwepa majukumu yake kama baba.
Shaz anasema jambo hilo lilimfanya amtumie maafisa wa usalama alipokuwa kwenye show huko Voi siku ya ijumaa wiki iliyopita.
Msanii huyo tayari amefikishwa kwenye mahakama ya watoto ya Tononoka.