Aliyekuwa member wa kundi la Destiny’s Child, Kelly Rowland amenyoosha maelezo kufuatia uvumi kwamba kundi la Destiny’s Child lipo mbioni kuerejea kwa ajili ya kufanya muziki mpya na tamasha lao la muziki.
Kupitia mahojiano na Entertainment Tonight, Kelly Rowland amesema kundi hilo kwa sasa linaendelea kuweka mikakati ya kurejea kwenye muziki huku akiwataka mashabiki wao kukaa mkao wa kula kuwapokea.
“Tunampenda kila mtu sana ila nadhani jambo hili linastahili kuwa la kushtukiza zaidi, kila kitu kitapangwa ila mtashtukizwa tu, itakuwa surprise mzuri”.
Kundi hilo linaloundwa na mastaa watatu akiwemo Beyonce, Kelly Rowland na Michelle Williams lilivunjika mwaka 2006 na kila msanii akaendelea kufanya kazi zake za muziki kama msanii wa kujitegemea.