You are currently viewing Kelly Rowland amkingia kifua Chris Brown kwenye Tuzo za American Music Awards

Kelly Rowland amkingia kifua Chris Brown kwenye Tuzo za American Music Awards

Mwanamuziki Kelly Rowland amemkingia kifua Chris Brown mbele ya mashabiki ambao walianza kumzomea kwenye utoaji wa Tuzo za (American Music Awards) usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kumtangaza kama mshindi wa kipengele cha Msanii Bora wa R&B, Breezy hakuwepo ukumbini na Kelly alilazimika kumchukulia Tuzo hiyo, lakini wakati akizungumza, mashabiki walianza kumzomea.

Kelly Rowland aliwakatisha na kuyasema mazuri ya Chris Brown. Utakumbuka siku chache kuelekea utolewaji wa Tuzo za American Music Awards, Waandaaji wa tuzo hizo waliifuta performance ya Chris Brown ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya kutoa heshima kwa Michael Jackson.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke