Rapa Kendrick Lamar ameendeleza ubunifu wake wa kutumia sura za watu mbalimbali kwenye mwili mmoja ‘Deepfake’ katika kufikisha ujumbe anaoutaka.
Kama alivyofanya katika wimbo wake wa “The heart part 5” uliopo kwenye album yake ya “Mr Morale & the Big Steppers” ambapo alitumia sura za watu mbalimbali maarufu kama Kanye West, Will Smith na Nipsey Hussle.
Rapa huyo ametumia ubunifu huo katika kutambulisha ngoma yake ya “Saviour” kwenye tamasha lililofanyika Paris wiki hii ambapo ametumia sura ya J Cole, Future pamoja na Lebron James.