Baada ya ukimya wa takribani miaka 5, rappa Kendrick Lamar anarudi kwenye masikio yako.
Kupitia mitandao yak ya kijamii Lamar ametangaza rasmi ujio wa Album yake mpya iitwayo “Mr. Morale & The Big Steppers” ambayo itaachiwa rasmi Kesho Mei 13.
Rapa huyo kutoka marekani ameachia Cover ya Album yake mpya “Mr. Morale & The Big Steppers” ambapo ameonekana akiwa amevalia crown yenye miiba, bastola kiunoni huku akiwa amembeba mtoto wake wa Kike.
Mbele yake anaonekana mkewe Whitney Alford akiwa amekaa kitandani akimbembeleza mtoto wao mwingine.
Album hii mpya itatoka chini ya lebo yake binafsi ‘PG Lang’ kwa ushirikiano na Top Dawg Entertainment.
Ikumbukwe, “Mr. Morale & The Big Steppers” inaifuata albamu yake iitwayo “DAMN” iliyotoka mwaka 2017.