You are currently viewing KENRAZY AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA CHAMA CHA KISIASA CHA ODM KISA MALIPO DUNI

KENRAZY AAPA KUTOFANYA KAZI TENA NA CHAMA CHA KISIASA CHA ODM KISA MALIPO DUNI

Staa wa muziki nchini Kenrazy amefunguka namna alivyolipwa malipo duni na chama cha kisiasa cha ODM wakati wa kampeni za urais mwaka wa 2013.

Akihojiwa na Iko Nini, Kenrazy amesema alikuwa na matarajio makubwa kutoka kwa chama hicho kwani aliandamana nao kwenye kampeni zao nyingi.

Hitmaker huyo wa “Mbilikimo Mkora” amesema licha ya kutumbuiza kwenye misafara tofauti za kampeini ya chama cha ODM alilipwa shillingi elfu 70 kwenye mkutano wa mwisho wa chama hicho katika bustani ya Uhuru.

Rapa huyo amesema ‘malipo hayo duni’ yamemfanya kutofanya kazi tena na chama cha ODM ambapo amedokeza kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu atafanya biashara na chama kingine cha kisiasa ambacho kitamlipa vizuri

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke